Tarehe 12 Aprili, 2018
Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga alifanya ziara katika kituo cha
kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet; KOJ) kilichopo jijini Dar es
Salaam, lengo likiwa ni kukagua shughuli zinazotekelezwa na kituo hicho pamoja
na kutatua changamoto mbalimbali.
Katika ziara hiyo Mhandisi Luoga aliambatana
na Kamishna Msaidizi wa Petroli, Mhandisi Mwanamani Kidaya, wataalam kutoka
Idara ya Nishati na mwakilishi kutoka Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja
(PBPA).
Kamishna Luoga
alielekeza kituo hicho kuendelea kuimarisha ulinzi ili kudhibiti upotevu wa
mafuta. Aidha alielekeza kituo hicho kuendelea kushirikiana na wadau wengine
kwa karibu zaidi katika kuboresha shughuli zake.
Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (katikati) akielekeza jambo katika sehemu ya kupokea mafuta aina ya petroli na dizeli katika kituo hicho. |
Sehemu ya gati za
kupokea mafuta katika kituo cha kupokea mafuta cha Kurasini (Kurasini Oil Jet;
KOJ) kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
|