Monday 5 March 2018

Katibu Mkuu wa Nishati akutana na Kampuni ya Rift Valley Energy

Na Zuena msuya Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamis Mwinyimvua amekutana na Kampuni ya Rift Valley Energy inayotaka kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya upepo Mkoani Njombe.

Dkt.Mwinyimvua amekutana na Kampuni hiyo katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati Mkoani Dodoma.



Katika mazungumzo hayo Kampuni hiyo imesema kuwa mbali na kutaka kuzalisha Umeme wa upepo, tayari kampuni hiyo inazalisha umeme wa Megawati 4 kwa kutumia maporomoko ya maji katika eneo Mwenga mkoani Njombe na kuusambaza kwenye vijiji 34 vinavyozunguka eneo hilo.

Aidha kampuni hiyo pia itatekeleza miradi mingine ya umeme kwa kutumia maporomoko madogo ya katika maeneo ya Luponda Mkoani Njombe na Suma Mkoani Mbeya.